KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison, ameibuka na jipya akisema kwamba, sababu kubwa ya yeye kutoenda mazoezini ni kuhofia kupigwa na mashabiki na wachezaji wenzake wa Yanga.
Mbali na hilo la kupigwa, Morrison amesema pia kitendo cha mkataba wake kumalizika, ndiyo kimechochea zaidi yeye kutoungana na wenzake mazoezini hadi sasa.
Morrison ambaye Julai 12, mwaka huu katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba, aliondoka uwanjani mara tu alipofanyiwa mabadiliko huku timu yake ikifungwa mabao 4-1.
Tangu siku hiyo, hajaungana na wenzake hadi leo huku akisema mkataba wake umemalizika Julai 15, mwaka huu. Nyota huyo raia wa Ghana, alijiunga na Yanga, Januari mwaka huu.
Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison amesema: “Nimechoshwa kabisa na hali ya maisha ndani ya Yanga kwani mambo yanayoendelea kwangu na uongozi yanafanya hadi kutoelewana na nyota wenzangu.
“Nimesikia kuwa walipanga kunifanyia fujo mazoezini na ndiyo maana nikaona kwa kuwa mkataba wangu umemalizika ni bora nikae pembeni hadi pale nitakapopata muafaka wa madai yangu na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania),” alisema Morrison.







Kwa nini uongozi wa Yanga hauchukui maamuzi magumu?si wamuache aende kokote anapotaka?Tujiulize kabla yake yeye kuna mafundi wangapi walipita hapo tena zaidi yake?Ameshatuonesha kidole cha kati mwisho wa yote atatuvua suruali.Mnafuga ugonjwa ambao ukikomaa utakosa tiba mwisho wa yote itakuwa ni kukata kiungo
ReplyDeleteHatuwezi kumuachia kijingajinga bila pesa yetu kurudishwa,timu inayomtaka ilete ofa tutawaachia hatuna tatizo.
DeleteWewee hajapewa fungu na mishahara anadai miezi miwili.Muhimu ni kumuacha aondoke
DeleteKinachofurahisha jina ka muuaji wa Simba lime expire tarehe 12 July 2020.Ahsante wachezaji wa Simba kwa kukatisha ngebe za globu hii kwanza na Utopolo kwa ujumla.
ReplyDeleteNi kweli au sio kweli kuwa GSM walimpa mkataba wa miaka miwili???????......au ilikuwa galagaja..
ReplyDelete