July 14, 2020


LUIS Miqussone, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni kuona wanaendelea kupata ushindi Kwenye mechi ambazo zinafuata ikiwa ni pamoja na mchezo wa fainali dhidi ya Namungo FC.

Mchezo huo wa fainali wa Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa Agosti mbili, Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Namungo iliyo chini ya Kocha Mkuu,  Hitimana Thiery ilitinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars, uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Miqussone alifunga moja ya bao wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 ambao ulikuwa ni wa hatua ya  nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Taifa.

"Nimefurahi kufunga mbele ya Yanga na kuona timu yangu inasonga mbele mpaka hatua ya fainali,  kwetu sisi tutaendelea kupambana ili kufikia malengo yetu.

"Tangu awali tulikuwa tunahitaji kupata ushindi mbele ya Yanga kwa kuwa imetokea basi tunasonga mbele kwa juhudi kusaka ushindi zaidi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic