BOURNEMOUTH FC inayonolewa na Eddie Howe jana iliishushia kichapo cha mabao 4-1 Leicester City Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Vitality.
Leicester City ilianza kupachika bao dakika ya 23 kupitia kwa Jamie Vardy ambalo lilisawazishwa dakika ya 66 na Junior Stanislas kwa mkwaju wa penalti.
Moto uliendelea dakika ya 67 kupitia kwa Dominic Solanke aliyetupia mabao mawili jingine alitupia dakika ya 87 huku bao moja Jonny Evan's akijifunga dakika ya 83.
Bournemouth imeishusha timu ya Aston Villa ya Mbwana Samatta kwa kuwapunguzia kasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu England.
Villa imeshushwa nafasi ya 18 mpaka 19 baada ya Bouremouth kufikisha pointi 31 huku Villa ikiwa nafasi ya 19 na pointi 30 zote zimecheza mechi 35.
0 COMMENTS:
Post a Comment