July 13, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa haikuwa bahati yao jana kushinda mbele ya Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuchapwa mabao 4-1 mbele ya Simba.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa ulikuwa na ushindani mkubwa  ambapo Simba walianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kipindi cha pili Yanga nao waliweza kubadili upepo wa mchezo.

Simba walipata bao la kwanza dakika ya 21 kupitia kwa Gerson Fraga ambalo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko na kipindi cha pili Simba ilifunga mabao matatu.

Alianza Clatous Chama dakika ya 50, Miquissone dakika ya 52 na lile la nne lilifungwa na mzawa Mzamiru Yassin na lile la Yanga likifungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum,'Fei Toto'.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa makosa yao yamewagharimu hivyo wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

"Tumeshindwa kwenye mchezo wetu hilo lipo wazi lakini haina maana kwamba msimu ujao tutashindwa kufanya vizuri.

"Kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao ili kuwa bora zaidi kwani kila kitu ni mipango tunaamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Mwandishi unasemaje yanga walibadili upepo kipindi cha pili wakati ndani ya kipindi hicho walifungwa goli tatu? Tuwe wakweli, kwa mchezo wa jana yanga walizidiwa dakika zote 90

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anafanana na mwandishi wa itv wa michezo wanaweka ushabiki mbele

      Delete
  2. Hawana la kusema isipokuwa makosa waliyoyafanya ndiyo yaliyowanyima ushindi lakini hawataji makosa yenye we. Safari hii hata wameshindwa kutaja visingizio walivovizowea kua Simba imebebwa kwa mara ya Kwanza. Hamna jipya na bora mnyamaze tu.

    ReplyDelete
  3. Ukiikamata midfield ya Simba kszi imekwisha-Antonio Nugaz. Sasa sijui jana kimeshindikana nini?Si ilikuwa rahisi tu kuikamata midfield ya Simba!!!

    ReplyDelete
  4. Yule jamaa wa ITV ndio hamna kitu kabisa yule hafai kabisa hata kuwa mwandishi

    ReplyDelete
  5. Waandishi andikeni facts sio ushabiki. Vyombo vingi vya habari tokea jana usiku vimepoa kabisaaa...
    Uwezo wa timu bora umeonekana uwanjani na sio redioni wala magazetini. Mtani tengenezeni timu na muwache kusajili etii wachezaji tisa wapya kwa ajili ya mtani wako lol...🤦

    ReplyDelete
  6. Kazi yao kuwasifia hao ngedere GONGOWAZI hivyo vyombo vya habari na huyo msemaji wao asio ujuwa mpira kazi kutowa ngonjera mwambie sasa atowe ngonjera zake mshamba huyo watakuwa nafasi ya 7 sasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic