July 13, 2020




TOTTENHAM Spurs iliyo chini ya Kocha Mkuu, Jose Mourinho ilishinda mabao 2-1 mbele ya Arsenal jambo ambalo limempa kiburi meneja huyo kwa kusema kuwa hakufikiria kuwafunga wapinzani wake.

Son Heung-min nyota wa Tottenham Hotspur dakika ya 19 alisawazisha bao lililofungwa na Alexandre Lacazette wa Arsenal dakika ya 16 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana.

 Spur ilipata bao la pili lililofungwa dakika ya 81 lililofungwa na Toby Alderweirled na kuwafanya wasepe na pointi zote tatu Uwanja wa Tottenham 

Ushindi huo unaifanya Spurs ifikishe jumla ya pointi 52 ikiwa nafasi ya 8 huku Arsenal ikiwa na pointi 50 zote zimecheza mechi 35.

Mourinho amesema kuwa kuna umuhimu wa wachezaji wake kupambana zaidi kufikia malengo ambayo wanahitaji na haikuwa kipaumbele kushinda mchezo huo ila wachezaji wametimiza majuku yao na ni kazi yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic