MSHAMBULIAJI namba moja wa Klabu ya Simba Meddie Kagere amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/20.
Kagere alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Paulo Nonga wa Lipuli na Never Tigere wa Azam FC alioingia nao fainali.
Kagere ametupia jumla ya mabao 19 na anaongoza kwenye ligi huku Nonga akiwa na mabao 11.
0 COMMENTS:
Post a Comment