Manchester City, imeshinda rufaa yake iliyokata kutokana na kufungiwa kutoshiriki miaka miwili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
City ilipinga maamuzi ya kufungiwa kushiriki michuano hiyo mikubwa baada ya kufungiwa mwezi Februari kutokana na kukiuka matumizi ya fedha kwenye masuala ya usajili.
Ligi Kuu England wamethibitisha kuwa walifanya makosa kwenye maamuzi yao na wamejiridhisha baada ya kufuatilia upya masuala hayo.
Baada ya kupitia ushahidi na vigezo muhimu katika kusikiliza rufaa hiyo ya City waliopoteza ubingwa msimu huu ambao umebebwa na Liverpool.
Ushahidi huo umeskilizwa kwa muda wa siku tatu kwa mwezi Juni na kwa sasa City wapo huru kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Jumamosi waliishushia kichapo cha mabao 5-0 Brighton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 72 kibindoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment