July 14, 2020


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa iwapo ingetokea timu yake ingefungwa mbele ya Yanga, Julai 12 alikuwa amepanga kuhama nchi ya Tanzania kwa muda.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga, kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Taifa. 

Mabao ya Simba yalifungwa na Gerson Fraga kwa pasi ya Chama, Clatous Chama akimalizia pasi ya Bocco, Luis Miqussone kwa pasi ya Papy Tshishimbi na Mzamiru Yassin huku lile la Yanga likifungwa na Feisal Salum kwa pasi ya Jonas Mkude. 

Manara amesema:" Ulikuwa mchezo mgumu na wenye ushindani kwelikweli ila ninasema wazi kuwa endapo tungefungwa tu basi nilikuwa ñimepanga kuondoka Dar kwa ndege iliyokuwa inapaa muda wowote.

"Kwenda ingejulikana wakati huo ingekuwa Rwanda, Burundi ama Congo ingejulikana wakati huo nisingebaki Bongo kwa kweli maana wasingenipa raha watani zetu hawa acha kabisa.

"Lile bao moja tulilofungwa lilinipa tabu kweli sio mimi hata viongozi wenzangu nao pia walikuwa wanapata," amesema.

Simba itamenyana na Namungo FC ambayo ilikata tiketi kwa kushinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars. 

2 COMMENTS:

  1. Huyo hana huo ubavu. Ahame aende wapi, labda ahame dar aende kigoma. Kuhamia nchi nyingine kunahitaji kujipanga

    ReplyDelete
  2. Kuwapisha Gongonje kwa muda wa wiki tu, hakusema atahama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic