LIPULI FC leo, Julai 14 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Samora, Iringa.
Lipuli haijawa na mwendo mzuri baada ya masuala ya michezo kuendelea baada ya janga la Virusi vya Corona kuelezwa kuwa limepungua Kwenye ardhi ya Bongo.
Mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Alliance FC inakutana na KMC iliyotoka kushinda mabao 2-0 mbele ya Singida United.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 ikiwa imecheza jumla ya mechi 34 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kibindoni ina jumla ya pointi 37 ipo kwenye hatari ya kushuka Daraja iwapo itashindwa kuchanga karate zake vizuri kwenye mechi zilizobaki ambazo ni nne.
Msimu huu wa 2019/20 zinashuka jumla timu nne na mbili zitakazoshika nafasi ya 15&16 zitacheza play off na timu za Ligi Daraja la Kwanza.
Tayari Singida United imeshamalizana na suala la kubaki Kwenye ligi msimu huu ikiwa imejikusanyia pointi 15 baada ya kucheza mechi 34.
Mshambuliaji wao Daruesh Saliboko mwenye mabao 10 amesema bado wana nafasi ya kupambana kubaki kwenye Ligi msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment