July 21, 2020


NYOTA wa Yanga, Feisal Salum amesema kuwa iwapo Simba ama Azam watahitaji huduma yake hana tatizo nao kwa kuwa kazi yake ni mpira hana chaguo iwapo utaratibu utafuatwa.

Feisal amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Yanga akiwa na uwezo wa kufunga pamoja na kutibua mipango ya wapinzani wake.

Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho walipokutana na Simba wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 alimtungua Aishi Manula kwa pasi ya Jonas Mkude.

Pia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mbele ya Mwadui FC wakati wakilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa alimtungua mlinda mlango wa Mwadui FC, Mussa Mbissa kwa pasi ya Mrisho Ngassa.

"Mimi ni mchezaji na ikitokea nimepewa ofa iwe Simba ama Azam FC sina tatizo nitafanya kazi ila muhimu utaratibu kufuatwa nitafanya kazi," amesema.

11 COMMENTS:

  1. Asifikirie kwenda Simba atapotea kabisa, benchi litamuhusu, bora aendelee kua hapo hapo Yanga.
    Kwa.kiwango chake nawaza ataenda.kumuweka benchi nani kayika kikosi cha Simba

    ReplyDelete
  2. Mwandishi, mimi niliangalia mechi hiyo. Ukweli haikuwa pasi ya Jonas Mkude directly bali katika harakati za kuokoa Jonas alipiga mpira wa kichwa ukatua kwa Feisal ambaye wachezaji wa Simba walikuwa wamemuacha huru bila kumkaba. Mkude ni mpambanaji mzuri sana katika kikosi cha Simba na kwa hiyo ukweli uandikwe kuhusu anachokifanya uwanjani

    ReplyDelete
  3. Vipi unamsihi abaki Yanga na Bila ya shaka inaonesha keshachoka nako. Ana akili yake kwani yeye si mtoto mdogo

    ReplyDelete
  4. Huyo kwa kiwango chake Bado San kucheza Simba,n Bora abak yanga tu,,Simba n levo nyingne kabsa sshv

    ReplyDelete
  5. Atacheza namba ngapi Simba?Uwezo wake ni level ya Yanga au Azam lakini sio Simba.
    Simba kwa midfielders ni level nyingine.

    ReplyDelete
  6. Kwa Simba atasuguwa mbao Hana kiwango kinavhohitajika Katika kikosi cha Sven

    ReplyDelete
  7. Atakuwa anawatisha yanga wampandie dau, ukweli simba hapati namba

    ReplyDelete
  8. Aje kwa ajili ya mechi mbili , kwanza ni ile kwenye simba day ambayo wachezaji wote hupatiwa nafasi na mechi nyingine labda kwenye mapinduzi cup

    ReplyDelete
  9. ww unaesema hana kiwango hujui mpira ukweli watu wamekuwa wakisema wakiponda wachezaji huku wanasahau ukweli halisi hapana shaka kusema kuwa viungo bora kutoka tz ni feisal salum fei toto na awesu awesu. acha unazi wa timu unazozipenda ebu toa kile unachokiona kwenye mguu wa hawa vijana. fei dk alizopewa kwenye timu ya taifa ni zaidi ya unavyomuongelea au napata shaka na jinsi ulivyokwenye tasnia ya mpira

    ReplyDelete
  10. mchezaji kuwa yanga na azam fc si kwamba hawajui mpira ebu angalia kikosi cha simba kimeundwa na wachezaji kutoka timu gani mf. mzuri ni bocco; manula; kapombe; erasto nyoni; pascal wawakuna gadiel michael nk wengine mmewatoa mtibwa fc kama vile kichuya' hasan dilunga; nk

    ReplyDelete
  11. ww unaesema hana kiwango hujui mpira ukweli watu wamekuwa wakisema wakiponda wachezaji huku wanasahau ukweli halisi hapana shaka kusema kuwa viungo bora kutoka tz ni feisal salum fei toto na awesu awesu. acha unazi wa timu unazozipenda ebu toa kile unachokiona kwenye mguu wa hawa vijana. fei dk alizopewa kwenye timu ya taifa ni zaidi ya unavyomuongelea au napata shaka na jinsi ulivyokwenye tasnia ya mpira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic