July 21, 2020



SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa watatutumia nguvu kubwa sana kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya fainali mbele ya Namungo, inayotarajiwa kuchezwa Agosti 2,kutokana na Uwanja kutokuwa na ubora wa kisasa.
Simba itakutana na Namungo FC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa ingependeza zaidi iwapo waandaaji wa Kombe la Shirikisho wangechagua uwanja mmoja maalumu kwa ajili ya kombe hilo ambalo lina heshima tofauti na kuupeleka kila mkoa.
“Waandaaji wamefanya jambo zuri kupeleka mchezo nje ya Dar es Salaam lakini wanapaswa waangalie kwamba kuna mazingira ambayo yatakuwa si rafiki kwa wachezaji hasa kwenye mchezo mkubwa kama fainali kupelekwa Sumbawanga kwenye uwanja ambao unaanza kufanyiwa marekebisho kwa sasa.
“Ninadhani itakuwa fainali ngumu na wachezaji hawatatoa burudani ile ambayo imezoeleka kama ingekuwa pale Uwanja wa Taifa, hivyo wakati mwingine ningependa kuwashauri hawa waandaaji wawe na sehemu maalumu ya kuchezea fainali ya mashindano haya makubwa, wachague tu hata taifa pale ujue mchezaji kucheza ni CV,” amesema Matola.
Simba ilitinga hatua hiyo kwa kushinda mabao 4-1 mbele ya Yanga Uwanja wa Taifa, huku Namungo ikiibukia fainali baada ya kushinda mbele ya Sahare All Stars bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

4 COMMENTS:

  1. Hao TTF Wakati mwengine tia maji tia maji na yote inatokana na kukosa ubunifu Ingawa kweli tupo kwenye mhemko wa corona lakini kwa nini waupeleke mchezo mkubwa kama wafainali kwenye uwanja mb'ovu?

    ReplyDelete
  2. mpira wa tanzania unatajiwa usimamiwe na watu ambao walishawahi kicheza mpira

    ReplyDelete
  3. Siamini kama ubora wa uwanja wa kambarage Rukwa utakua na ubora wa uwanja kama wa Taifa.. nina imani kiwango cha uchezaji hakita kua kizuri kutokana na ule uwanja ambao unafanyiwa marekebisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic