July 30, 2020


BENCHI la Ufundi na Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kwa pamoja wamekubaliana kumbakisha kiungo mkabaji raia wa Brazil, Gerson Fraga.

Kiungo huyo ni kati ya wachezaji waliokuwa wakihusishwa kuachwa Simba katika kuelekea msimu ujao akiwemo na Mbrazili mwenzake, Tairone Santos ambao walijiunga pamoja mwanzoni mwa msimu huu.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo hataachwa kama ilivyokuwa imepangwa na badala yake ataendelea kukipiga tena kwenye msimu ujao.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiungo huyo amebakishwa baada ya kuona kiwango kikibadilika kila siku kadiri anavyoendelea kucheza mechi ikiwemo na watani wao wa jadi, Yanga ambayo Mbrazili huyo alifunga bao.

Simba ilishinda mabao 4-1 mbele ya Yanga Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya nusu fainali. Bao la ufunguzi lilifungwa na Fraga akimalizia pasi ya Clatous Chama jambo lililomuongezea thamani ndani ya klabu hiyo.

Aliongeza kuwa wakati kiungo akibakishwa, mwenzake Tairone yeye ataachwa kwenye usajili wa msimu ujao kwa kuusitisha mkataba wake wa miaka miwili aliousaini.

“Fraga kadiri siku zinavyokwenda anaonekana kuzidi kubadilika kwa kuonyesha kiwango kikubwa, mfano mzuri mchezo wetu na Yanga alicheza kwa kiwango kikubwa ambacho kiliwashtua viongozi.

“Hivyo, basi kutokana na kiwango hicho alichokionyesha wamekubaliana viongozi na benchi ka ufundi kuendelea naye katika msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Senzo Mazingisa kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Muda wa usajili bado, hivyo wachezaji wapya tutakaowasajili na tutakaowaacha tutatangaza.”

8 COMMENTS:

  1. Hamna mchezaji hapo wa kucheza michuano ya kimataifa,n Bora wawaache tu wite waondoke zao

    ReplyDelete
  2. Hata mpira wenyewe sijui kama unaujua wewe, mim nafikiri nyinyi ndo wale wakufuata mkumbo mnataka mchezaji mpaka awe anapiga chenga nyingi ndo unafikiri ni mchezaji.

    ReplyDelete
  3. lbda nikusaidie we iliyekoment wa kwanza hakuna kiungo bora vpl kwa sasa kama fraga nadhan upira ulianza kushabikia ukubwan

    ReplyDelete
  4. Huyo ni Utopolo. Fraga toka amepewa nafasi walinzi wa Simba wamepata ahueni kubwa.Anafanya majukumu yake kwa ustadi mkubwa.

    ReplyDelete
  5. Fraga ni kiungio bora sio Tanzania tu bale East Africa kwa sasa. Hachezi na majukwaa sababu kajifunza akiwa na Neyma! Huyo jamaa aliyetoa comment ya kwanza juu HAJUI MPIRA. NAHISI ANAFIKILI KUPIGA CHENGA NDIO KUJUA MPIRA! Amechemka atuachie Fraga wetu kiungo bora

    ReplyDelete
  6. Huyo Fraga mwanzoni sikumwelewa kabisa nikawa nashangaa Simba ilimuokota wapi mchezaji bomu namna ile. Lakini baada ya kupewa nafasi yakucheza mara kwa mara na kuzoea ligi yetu lazima nikiri huyo jamaa ni bonge la kiungo ameziba nafasi ya Kotei VIZURI. Katika mechi zote alizocheza kwa kweli ameficha udhaifu wa mabeki wa kati wa Simba. Lakini Simba isijisahau lazima isajili mabeki wa kati wa uhakika isitegemee kila siku tu Fraga atakuwa anaficha hayo madhaifu ya beki zao wa kati kwani ipo siku itakutana na dhahama kama zile za AS Vita na AL Haly kwenye CL. Fragga ni mtu na nusu aisee.

    ReplyDelete
  7. fraga binafsi nilikuwa namwelewa kati ya wabrazil wote kikubwa alichonacho ni anticipation ya kiwango cha juu ambayo wachezaji wengi sana wa kiungo wa kukaba tz hawana anaweza kukadiria njia ya mpira nafasi ya tatu kabla haujafika na akaharibu shambulizi. anasoma sana move za wapinzani viungo wengi wanakaba kwa kukimbiza mpira baada ya pasi fraga anajua mpira utapita wapi unamkuta keshafika hii ni akili zaidi na kuonyesha tofauti ya kiwango asiyejua mpira hawezi kuliona hili akimtizama fraga atamchukulia poa ila jamaa sio wa kawaida

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic