July 12, 2020


JULAI 12, leo itakuwa kimya kwa muda kuangalia namna gani ni nani atakayevuka hatua ya nusu fainali na kutinga kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho.

Ni miamba miwili ya soka, Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wakiwa na mataji 21 kibindoni na Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria wakiwa na mataji 27.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na Namungo iliyokamilisha kazi jana kwa kushinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Hivi hapa vikosi vya miamba hii ya soka vinatarajiwa kuanza na data zao kamili zipo namna hii:-
Aishi Manula

Kipa namba moja ndani ya Simba, kwenye mechi 34 amekaa langoni kwenye mechi 25 za ligi na kwenye Kombe la Shirikisho amekaa mechi moja ya hatua ya robo fainali wakati Simba ikishinda mabao 2-0 mbele ya Azam FC.

Manula kwenye mechi zote mbili za msimu huu wa 2019/20 walipokutana na Yanga yeye alikaa langoni Januari 4 kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na Machi 8 wakati Simba ikilala kwa kufungwa bao 1-0.

Haruna Shamte

Kuumia kwa beki wa kulia, Shomari Kapombe mfalme wa kumwaga maji pembeni akiwa na pasi sita kwenye ligi na mbili kwenye Kombe la Shirikisho kunatoa fursa kwa Shamte kuchukua nafasi yake.

Amecheza mechi 13 za ligi kati ya 34 ambazo zimechezwa na Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Pascal Wawa
Beki kisiki ndani ya Simba, akiwa amecheza jumla ya mechi 26 za Ligi Kuu Bara na kwenye mechi zote mbili walizokutana watani hawa wa jadi aliyeyusha dakika zote 90 uwanjani. Ndani ya ligi ametumia jumla ya dakika 2,301 na ana pasi moja ya bao kati ya mabao 69
Mechi zake hizi hapa:- Kagera Sugar (90), Biashara United (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mbeya City (90), Tanzania Prisons (90), KMC (90), Ruvu Shooting (90), Lipuli (72), Yanga (90), Mbao (90), Alliance (90), Namungo (69), JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), Lipuli (90), KMC (90), Azam (90), Yanga (90), Singida United (90), Ruvu (90) Mwadui (90), Mbeya City (90) na Ndanda FC (90)

Erasto Nyoni

Kiraka wa Simba, mkongwe mwenye uwezo wa kucheza namba zaidi ya moja ndani ya uwanja. Akiwa kwenye ubora wake lazima safu ya ulinzi iwe imara.

Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao 69 ana bao moja kichwani aliwatungua Azam FC na alikosa mchezo mmoja wa Januari 4 kwa kuwa alikuwa na majeraha na mchezo wa Machi 8 alicheza kidogo na kupata majeraha kwa sasa yupo fiti.

Mohamed Hussein,’Tshabalala’

Nahodha msaidizi wa Simba ambaye anabebwa na spidi kubwa pamoja na maamuzi ya haraka ndani ya uwanja.
Uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao upo kwenye miguu yake ambapo amefunga jumla ya mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao.

Luis Miqussone
Wamempa jina la Mmakonde kwa kuwa anatokea karibu na watu wa Mtwara pale Msumbiji, ana uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga.

Ametumia dakika 863 kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, amecheza mechi 13 akiwa amefunga mabao matatu na pasi moja ya bao.

Hizi hapa mechi zake:-JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (16), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), KMC (75) Azam (83), Yanga (90), Singida United (90), Ruvu Shooting,(82), Mwadui (62), Mbeya City(35), Tanzania Prisons (23), Ndanda FC (72).
Jonas Mkude
Chaguo namba moja kwa makocha wote ndani ya Simba ambao wamewahi kupita hapo, hata Patrick Aussems alikuwa anasema kuwa hamna namna ikiwa Mkude atakuwa fiti lazima aanze.
Amefunga mabao mawili na ametoa pasi mbili za mabao, alionyesha uwezo wake kwenye mchezo wa robo fainali Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 2-0 kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha.

Gerson Fraga
Fraga ameanza kuaminika ndani ya Simba ambapo amecheza mechi nne mfululizo tofauti na mwanzo. Ametumia dakika 1,222 kwenye mechi za ligi akiwa amecheza mechi 17.
 JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (90), Azam FC (90), Singida United (9), Mwadui (90), KMC (90), Ruvu Shooting (90), Alliance (17), Coastal Union (90), Polisi Tanzania (90) JKT Tanzania (63), Singida United (38), Mwadui (90) Mbeya City (90) Tanzania Prisons (90) na Ndada FC,(72).
Meddie Kagere
Mtambo wa mabao ndani ya Simba akiwa na mabao 19 na pasi tano akiwa ametumia dakika 2,429 kwenye ligi. Kwenye mchezo wa Januari 4 wakati Yanga ikipindua meza kibabe kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 alifunga bao na kutoa pasi pia.Kwenye kombe la Shirikisho ana bao moja.
Mechi zake ni:-JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (87), Biashara United (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mwadui FC (90), Mbeya City (90), Prisons (90), KMC (90), Ruvu Shooting (75), Lipuli (90), Yanga (68), Mbao (90), Alliance (90), Namungo (90), Coastal Union (90), Polisi Tanzania (14), JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), Lipuli (79) na Azam (29), Yanga (69), Singida (90), Ruvu Shooting (90), Mwadui (28), Tanzania Prisons (90), Ndanda,(22) na Namungo,(90).

John Bocco
Nahodha wa Simba kwenye mchezo wa robo fainali alifungua mlango wa mabao kwenye ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa.
Kibindoni ana mabao saba ndani ya ligi na ni mshambuliaji pekee mzawa aliyefunga zaidi ya mabao 100.
Clatous Chama
Uwezo wake kwenye miguu ndio unaamua matokeo ya Simba yawe namna gani. Ana jumla ya pasi 10, na mabao matano. Amefunga mawili kwenye ligi na matatu kwenye Kombe la Shirikisho, pasi nane kwenye ligi na mbili kwenye Kombe la Shirikisho.
 
Hili hapa kosi la Yanga la ushindi litakuwa namna hii:-
Metacha Mnata
Kwenye mechi nne za Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikicheza jumla ya mechi nne alikaa langoni kwenye mechi tatu huku Farouk Shikhalo akitumia dakika 90 langoni.
Mnata ameonekana kupewa mikoba ya kuivaa Simba kwani kwenye mchezo uliopita wakati Yanga ikishinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar aliwekwa benchi na ndivyo ilivyokuwa pia kwenye mchezo uliopigwa Machi 8, Mnata aliwekwa benchi kuwapoteza maboya akaibukia Uwanja wa Taifa.

Jaffar Mohamed
Kiraka wa Yanga ambaye aliibuliwa na Kocha Mkuu wa zamani, Mwinyi Zahera aliwabana mbavu Meddie Kagere na John Bocco kwenye mchezo wa Machi 8 jambo linalompa nafasi ya kuanza jumla kwenye kikosi cha kwanza Julai 12.

Juma Makapu
Huyu ni kipenzi cha Luc Eymael ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga. Amekuwa akimpa nafasi kwenye mechi zake nyingi na ngumu huku naye akionyesha kwamba anaweza kufanya kazi yake kwa umakini.

Lamine Moro
Beki kisiki ambaye ni mbabe huyu amekuwa na uwezo mkubwa kwenye mechi zake nyingi ambazo anapewa nafasi.
Walipokutana na Simba ndani ya Ligi Kuu Bara alikuwa kisiki ndani ya klabu hiyo ambayo inapambana kusaka nafasi ya kimataifa.

Juma Abdul
Fundi wa kumimina maji ndani ya Yanga huku akipenda kutumia mguu wa kulia, Ana jumla ya pasi sita kwenye mguu wake wa kulia.
Yupo fiti kuwavaa wapinzani wake Simba akiwa ni nahodha msaidizi ndani ya kikosi hicho. Alikuwa akivuta pumzi wakati wachezaji wenzake wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar.

Haruna Niyonzima
Kwenye mchezo dhidi ya Biashara United uliopigwa Julai 5 aliumia goti ila Eymael amesema kuwa kwa hali aliyonayo kwa sasa anaongeza asilimia 50 kumpata sawa na ile ya kumkosa ndani ya uwanja.
Alifunga bao lililoipeleka Yanga hatua ya robo fainali kwa kuitungua Gwambina FC bao akiwa nje ya 18 kwenye ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.Uzoefu wa dabi unambeba pia.
Feisal Salum
Mzawa huyu ni fundi wa kupiga mashuti ya mbali na mvuruga mipango muda wote ndani ya yanga.
Machi 8, Chama aliomba poo kwa shughuli aliyokutana naye na alimchezea rafu ambayo baadaye aliweza kuomba msamaha kwa Fei Toto pamoja na mashabiki.

Kelvin Yondani
Kisiki ndani ya Yanga, mkongwe ambaye ana uzoefu na dabi zote kwa sasa na kiboko ya mtupiaji namba moja wa Simba, Kagere ameanza kupewa nafasi na Eymael ambaye mwanzo alikuwa hamuelewi.
Bernard Morrison
Nyota wa Yanga alikuwa kwenye mvutano mkubwa na Yanga kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni ishu ya mkataba ila kwa sasa mambo yapo sawa na amerejea kambini.
Bao lake alilomtungua Aishi Manula, Uwanja wa Taifa Machi 8 wakati Yanga ikishinda bao 1-0 ni moja ya mabao yake yanayokumbukwa kati ya mabao matano aliyonayo na pasi zake tatu.
Manne amefunga kwenye ligi na bao moja amefunga kwenye Kombe la Shirikisho,

Ditram Nchimbi
Msumbufu ndani ya Uwanja, Januari 4, Pascal Wawa hakuwa na chaguo zaidi ya kutumia nguvu kumzuia mwamba huyu mzawa ambaye amefunga jumla ya mabao sita na pasi tatu za mabao.
Anashikilia rekodi ya kufungua pazia kwa kufunga hat trick kwenye Ligi Kuu Bara aliwafunga Yanga ambao kwa sasa ni mabosi zake zama hizo alikuwa akikipiga ndani ya Polisi Tanzania.
David Molinga

Mtambo wa mabao ndani ya Yanga ni kinara kwa sasa akiwa na mabao 10. Uwezo wake wa kupiga vichwa na mipira iliyokufa vinampa nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa Julai 12.
Mchezo wake uliopita mbele ya Kagera Sugar wakati wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 alitoa pasi ya bao kwa lililofungwa na Morrison hivyo yupo kwenye moto.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic