July 21, 2020


CLATOUS Chama, kiungo wa Simba amesema kuwa isingekuwa mpira angejihusisha na masuala ya vichekesho kwani ni miongoni mwa vitu ambavyo alikuwa akifikiria kuvifanya wakati anakua.

Chama amekuwa kwenye ubora wake msimu huu kwa upande wa kuichezesha timu ya Simba ambapo akiwa bora ndani ya uwanja Simba huwa katika kasi yake na akipoa timu pia imekuwa ikipoa.

Kibindoni ana jumla ya pasi tisa ndani ya Ligi Kuu Bara na akiwa amefunga mabao mawili pia kwenye ligi.

Ameendelea kuwa kipenzi cha Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck pamoja na mashabiki wa Simba kutokana na juhudi zake ndani ya uwanja.

Chama amesema:"Zama zile wakati ninakua nilikuwa ninafikiria kufanya masuala ya vichekesho kwa kuwa ni vitu ambavyo ninapenda pia ila kwa kuwa nipo kwenye mpira maisha yangu yanaendelea hukuhuku."

3 COMMENTS:

  1. Mnawasikia waliopoa na wasio na zomeazomea, makelele wala malalamiko na raha kutawala

    ReplyDelete
  2. Wanazichanga faranga tu daah hazdi raha wapiganaji wa Simba akeeee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic