July 23, 2020


LIVERPOOL usiku wa kuamkia leo imeibuka na ushindi wa mabao 5-3 mbele ya Chelsea wakati wakikabidhiwa Kombe lao la Ligi Kuu England.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Anfield ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo timu zote zilikuwa zinahitaji ushindi ili kufikia malengo yao.

Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp ilikuwa inahitaji heshima kwani ilishamaliza kazi ya kusaka taji huku Chelsea inasaka nafasi ya kumaliza ndani ya tano bora.

Mvua ya mabao ilianza kumiminwa dakika ya 23 kupitia kwa Naby Keita ikaongezewa kasi na Trent Alexander-Arnold dakika ya 38 na Georgino Wijnaldum dakika ya 43 kwa upande wa Liverpool huku Olivier Giroud akiwatikisa dakika ya 45 kwa upande wa Chelsea.

Kipindi cha pili Chelsea walikuwa na kasi ya kutaka kuweka mzani sawa mambo yakazidi kuwa magumu dakika ya 55 Robert Firmino alipachika bao la nne kwa Liverpool na dakika ya 61 Tammy Abraham alicheka na nyavu kisha dakika ya 73 Christian Pulisic alifunga bao la tatu na la mwisho kwa Chelsea.

Msumari wa mwisho wa Liverpool ulipachikwa dakika ya 84 na Alex 0xlade-Chamberlain na kuwafanya Chelsea wakubali kupigwa mkono.

Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa mpaka pale atakapomaliza mchezo wake dhidi ya Wolves ndio atajua nini amevuna.

Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe jumla ya pointi 96 ikiwa nafasi ya kwanza huku Chelsea ikiwa nafasi ya nne na pointi 63 zote zimecheza mechi 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic