July 23, 2020


FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Mbao FC amesema kuwa angepewa timu mapema isingekuwa kwenye hali ya kupambania kushuka daraja kama inavyofanya sasa.

Minziro ameweza kurejesha makali ya Mbao FC kwa sasa ambapo baada ya kukabidhiwa timu hajapoteza mchezo hata mmoja kati ya michezo saba.

Ushindi wake wa jana, Julai 22 wa mabao 3-0 mbele ya Namungo FC Uwanja wa Kirumba umezidi kuongeza ushindani wa timu ambazo zitashuka daraja ambapo mpaka sasa hakuna nyingine iliyoonesha dalili za kushuka mpaka pale zitakapomaliza mechi zao.

Ni timu moja tu ambayo ina uhakika wa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2020/21 ambayo ni Singida Unted yenye pointi 18 kibindoni baada ya kucheza mechi 37.

Mbao ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 42 ambazo ni sawa na zile za Mbeya City iliyo nafasi ya 15 itakayoshuka leo Uwanja wa Azam Complex kumenyana na Azam FC ikiwa nafasi ya tatu.

Minziro amesema:"Bado hatupo sehemu salama kwa sasa tunapambana kuona namna gani timu inaweza kubaki ila nina amini ningekabidhiwa timu mapema nisingekuwa kwenye presha kubwa hivi.

"Nilichokifanya ilikuwa ni kuinyoosha safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa ina matatizo makubwa kidogo kwa sasa tunakwenda na tunafanya vizuri nawapongeza wachezaji katika hili." 

Kinara wa utupiaji ndani ya Mbao FC ni Wazir Jr ambaye kibindoni ana mabao 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic