July 24, 2020


TETESI za soka zinaeleza kuwa Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania na mshambuliaji wa Klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza, Mbwana Samatta anahusishwa na uhamisho wa kutimkia Klabu ya Fenerbahçe ya nchini Uturuki.

Fenerbahçe ambayo imeanza kupanga kikosi chake kuhakikisha inakuwa imara katika msimu ujao imeonesha nia ya kutaka kumsajili Samatta aliyetua Villa Park mapema Januari mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa Aston Villa imeonesha utayari wa kumruhusu nyota huyo aliyetokea KRC Genk kuondoka.

Samatta alisajiliwa na Aston Villa baada ya kufanya vizuri nchini Ubelgiji lakini tangu ametua nchini Uingereza amekuwa hafanyi vizuri katika klabu hiyo iliyopo katika hati hati za kujinasua isishuke daraja.
Kabla ya kujiunga na Aston Villa kulikuwa na tetesi kuwa nyota huyo alikuwa pia akiwindwa na Fenerbahçe.

Villa kwa sasa ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 37 inahitaji kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya West Ham United, Julai 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic