July 19, 2020


Nahodha wa Gwambina FC,  Jacob Masawe amesema anamshukuru Mungu kwa hatua aliyofikia kwa sasa pamoja na ushirikiano kwa kila mmoja.

Jana Julai 18 amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza kutokana na juhudi zake pamoja na ushirikiano aliokuwa akionyesha ndani ya Ligi.

Timu yake ilipoteza taji la ubingwa wa jumla kwa kufungwa bao 1-0 na Dodoma FC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. 

Massawe amesema:"Kwa kila hatua ninamshukuru Mungu kwa kuwa haikuwa kazi rahisi kufika hapa bali uwezo wake hivyo sina budi kusema asante.

"Wachezaji wenzangu, uongozi kiujumla wote wanapaswa kupewa pongezi kwani tulikuwa bega kwa bega katika kila hali mpaka tulipofikia hapa."

Gwambina mkononi  ina tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kuwa vinara wa kundi B ndani ya Ligi Daraja la Kwanza. 

Kibindoni Massawe ametupia jumla ya mabao 10 akiwa ni mtupiaji namba mbili ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic