July 23, 2020



NICHOLAS Wadada, beki wa Azam FC, leo ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Mbeya City, majira ya saa 1:00 jioni.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa nyota huyo raia wa Uganda anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo.

"Wadada hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo kwa kuwa ana kadi tatu za njano hivyo atatumikia adhabu yake hiyo lakini hakuna kitakachoharibika.

"Kuna wachezaji wengi na wazuri ambao wana uwezo wa kufanya kazi kama yeye ndio maana halisi ya timu, tunahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kumaliza Ligi Kuu Bara nafasi ya tatu," amesema.

Wadada ametoa jumla ya pasi saba za mabao huku yeye akipachika bao moja ndani ya Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 66.

Azam FC Inapambania nafasi ya pili na Yanga ambayo ina pointi 69 kibindoni kwa sasa baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar jana, Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic