July 6, 2020


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison leo ameanza safari kuelekea Bukoba kuungana na wachezaji wenzake ambao wana mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Julai 8.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, kwa kufungwa mabao 3-0, utapigwa Uwanja wa Kaitaba.

Jana, Julai 5 wakati Yanga ikilazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United ilikosa huduma ya Morrison ambaye aliachwa Dar.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alisema kuwa iwapo atamhitaji Morrison kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar atawaambia viongozi wampeleke.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram Morrison amewaambia mashabiki wake kuwa habari Bukoba, niambieni kile ambacho sijaskia. 

Morrison amefunga jumla ya mabao matatu na kutoa pasi tatu ndani ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic