UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa unandaa majeshi ambayo yataiangamiza Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara watakapokutana Julai 15 Uwanja wa Gairo.
Mtibwa Sugar imekuwa kwenye mwendo wa kususua kwani imetoka kuchapwa mbele ya Mbao FC ambayo ipo nafasi ya 19 na pointi zake 35 ikipambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa wamekuwa kwenye hali mbaya jambo ambalo linawakasirisha wanaamini watauwasha moto mbele ya Azam FC.
“Tuna hasira tumefungwa bao 1-0 na Mbao inauma, bao lilikuwa jepesi sana na vijana walipambana ila kwa sasa tutakuwa Morogoro, pale Gairo lazima tutawasha moto wa kweli mbele ya Azam FC,” alisema.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 38 inamenyana na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 65 zote zimecheza mechi 34.
0 COMMENTS:
Post a Comment