July 13, 2020


MCHEZAJI wa zamani wa Yanga, Bakari Malima maarufu kama Jembe Ulaya amesema kuwa Yanga ilifanya makosa makubwa kuwaanzisha kikosi cha kwanza wachezaji watatu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Julai 12 Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Ushindi huo unaipa nafasi Simba kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho.

Itakutana na Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery, Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mchezo wa fainali.

Malima amesema:"Bernard Morrisons, Papy Tshishimbi na Jaffary Mohamed walikuwa hawapaswi kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo kwa kuwa walishindwa kuumudu mchezo kipindi cha kwanza.

"Pia kitendo cha Morrison kushindwa kutulia ndani ya uwanja na kuondoka jumla bila kukaa benchi hii sio sawa kwani anaonekana hana nidhamu jambo ambalo halitakiwi katika timu inayotafuta mafanikio.

"Bado kuna nafasi ya Yanga kufanya marekebisho katika kile ambacho kimetokea, wafanye usajili mzuri na waepuke zile janjajanja kwenye usajili jambo ambalo litawapa matokeo mazuri kwenye mechi zao zinazofuata," alisema.

5 COMMENTS:

  1. Kama umeshindwa kujijenga ujanani huwezi kujijenga uzeeni.

    ReplyDelete
  2. Ngonjera za muuaji wa Simba zime expire jana tarehe 12 July 2020.

    ReplyDelete
  3. Hata ligi mtamaliza mkiwa nafasi mbaya kwa style hii mnayoionyesha. Msitukane mamba wakati Mto wenyewe hamjauvuka. Itabaki historia,watani tengenezeni timu ya ushindani kimataifa ili tuwe na ligi bora kwa ukanda huu wa Afrika na ikiwezekana Afrika nzima...💪

    ReplyDelete
  4. Ushindi tulioupata sisi Simba, wangeliupata Akina Gongowazi pasingekalika na tazama walipopata ushindi wa goli moja walifanya kila aina ya vituko kwasababu hawakutegemea kutokana na udhaifu na unyonge walivokuwa nao. Ama kwa myama aliezowea ushindi baada ya ushindi mambo kimya na powa.

    ReplyDelete
  5. Hakuna timu hapo kazi magazeti yao kuwapamba kila asubuhi huyo morson aligusa mpira mara 2 GONGOWAZI aka vyura aka kandambili tena zlikuwa 7 bahati yenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic