July 13, 2020



JOHN Bocco nahodha wa Simba amesema kuwa pongezi nyingi za ushindi wao wa jana wa mabao 4-1 mbele ya Yanga zinarejea kwa mashabiki pamoja na wachezaji kiujumla.

Simba ilipata ushindi wake wa kwanza ndani ya msimu huu wa 2019/20 baada ya kupoteza mechi ya ligi iliyochezwa Machi 8,kwa kufungwa bao 1-0.

Mechi ya kwanza iliyochezwa Januari 4, Simba ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 jambo ambalo liliwapa hasira Simba.

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ulikuwa ni wa tatu kwa Simba kukutana na Yanga na kupata ushindi.

Bocco amesema:-"Sisi ndio Simba na sisi ndio mabingwa. Pongezi nyingi kwa wachezaji,benchi la ufundi,viongozi wetu pamoja na mashabiki."

Ushindi huo unaipa tiketi Simba kutinga hatua ya fainali ambapo itacheza na Namungo, Sumbawanga, Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic