July 22, 2020



MTIBWA Sugar leo imebanwa mbavu na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Morogoro kwa kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Haruna Chanongo alianza kufunga bao dakika ya 28 ila lilishindwa kuwapa pointi tatu mbele ya Yanga baada ya Adeyum Saleh kusawazisha bao hilo dakika ya 83.

Mchezo wa leo ulikuwa ni muhimu kwa Mtibwa Sugar kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja huku kwa Yanga ikiwa ni kwenye kuwaongezea ufalme nafasi ya pili.

Sare hiyo inawafanya Mtibwa Sugar na Yanga wagawane pointi mojamoja.

Yanga inafikisha pointi 69 ikiwa nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar wakifikisha pointi 42 nafasi ya 14 ambayo bado sio salama kwao kwa kuwa inaweza kufikiwa na Mbao FC yenye pointi 42 ikiwa itashinda mchezo wake wa mwisho.

Vita ya kushuka daraja inazidi kupamba moto huku Singida United ikitazama namna mambo yanavyokweda na kwenye mchezo wake wa leo imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar.

2 COMMENTS:

  1. Hamna timu hapo vyura aka GONGOWAZI aka kandambili wazee wa droo

    ReplyDelete
  2. Hawa watu wanavurugana toka chini mpaka juu na imepelekea sasa hata wachezaji kila mmoja anajiamulia anavotaka ende mazoiezini au asende ashiriki mechi au asishiriki inafika hadi kocha anafukuza baraza la ufundi Zima kutokana na vituko anavofanyiwa na huku baadhi ya nyota wakijiweka sokoni na anapoulizwa yukowapi mchezaji hujibu sijui Jee nini inakuwa hali ya muekezaji. Wachezaji wamepoteza morali na Wanapofugwa wanasema Refa kauza mechi, Simba kanunuwa mechi hakuna kuheshimiwa a fujo ndilo linalotawala na mwisho wake hauonekani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic