July 24, 2020


WAZIR Junior, mshambuliaji namba moja wa kikosi cha Mbao FC amesema kuwa kifo cha Benjamin Mkapa aliyekuwa rais wa awamu ya tatu kimeacha pengo kwa Afrika kutokana na mchango wake mkubwa kwenye jamii.

Usiku wa kuamkia leo, Julai 24, Rais wa Tanzania, John Magufuli alitangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Mkapa kilichotokea Dar wakati akipewa matibabu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wazir Jr amesema kuwa ni jambo gumu kulipokea ila kwa kuwa limetokea hakuna namna zaidi ya kushukuru.

"Kwanza kila kilichopo juu ya ardhi kitatoweka na utukufu wote anabaki nao Mungu wa milele, Mkapa alikuwa kiongozi makini kwa aliyoyaacha tutamkubuka.

"Uwanja wa Taifa ambao umepewa jina la Benjamin Mkapa upo vizuri ni huzuni kwetu na Afrika," amesema.

Jr ametupia mabao 12 ndani ya Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro ambaye ameonyesha utofauti kwa kuongoza kikosi hicho kwenye mechi saba bila kupoteza.

Mbao ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 42 baada ya kucheza mechi 37, kete yake ya mwisho Julai 26 dhidi ya Ndanda iliyo nafasi ya 19 na pointi 41.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic