July 13, 2020


GERALD Mdamu, mshambuliaji wa Mwadui FC amesema kuwa bado wana nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa wamekubaliana kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zilizobaki.

Mwadui imepokea kichapo kwenye mechi zake mbili za hivi karibuni ambapo ilipigwa mabao 3-2 na KMC na bao 1-0 mbele ya Azam FC mechi zote zikichezwa Uwanja wa Azam Complex.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wanazidi kupambana ili kuwa bora hivyo mashabiki waendelee kutoa sapoti.

"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi kwa hapa tulipo sio sehemu salama tutapambana kwa ajili ya mechi zetu zilizobaki.

"Wachezaji na benchi la ufundi linatazama namna ambavyo tunakwenda lakini hesabu zetu ni kuona kwamba tunarejea kwenye ubora bado tunazidi kuendelea kupambana," amesema.

Mwadui FC ipo nafasi ya 13 ikiwa imekusanya pointi 40 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mabatini Julai 14.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 44 zote zimecheza jumla ya mechi 34 ndani ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic