July 24, 2020


FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa ikiwa kuna jambo baya ambalo amelifanya ndani ya Yanga wamwambie kwa sasa kwa kuwa anabebesha mizigo isiyomuhusu kila wakati.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba miongoni mwa viongozi ambao wanaihujumu Yanga ni pamoja naye jambo ambalo limemfanya asiwe na furaha.

Mwakalebela amesema:"Nimekuwa nikiambiwa kwamba ninafanya mambo ambayo sio sawa na mambo yote mabaya ninaambiwa ni mimi katika hili mimi sina furaha kwa kweli.

"Nashutumiwa kwamba nimehujumu timu kwa kuchukua hotel ambayo ni ya watu wa Lipuli jambo ambalo mimi sijashirikishwa na sijui chocchote kuhusu timu kwa sasa.

"Kila baya la Yanga ninatajwa mimi, kwani nina nguvu gani ndani ya Yanga ya kuweza kufanya yote hayo? Ikiwa kuna jambo ambalo wanahitaji nifanye basi waniambie kwa sasa kwani sio sawa kupeana mizigo ambayo haina ukweli," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Sasa kama hakuna ya watu wa yanga wangelala nje?
    Acheni unprofessional reasons mtazidi kupotea!
    Angalieni madhaifu yenu mjirekebishe, mnang'ang'ania sababu za kizamaniii!

    ReplyDelete
  2. Jana Mkwasa, Leo Mwakalebela, utopolo y??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic