July 27, 2020


BAADA ya Yanga kutoa taarifa za kuachana na Luc Eymael kwenye nafasi ya benchi la ufundi, aliyekuwa Kocha Mkuu wa zamani wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameibuka na kumchana Mbelgiji huyo kuwa sio kocha.

Eymael ameachishwa kazi kutokana na vitendo vyake vya kibaguzi pamoja na matamshi yasiyo ya kiuungwana ambayo aliyasambaza jana, Julai 26 baada ya kumaliza kusimamia mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli na kushinda bao 1-0.

 Zahera amesema kuwa kwa mwenendo wa  Eymael ulivyokuwa hakuwa na maisha marefu ndani ya kikosi cha Yanga hata nje hawezi kudumu akipata timu.

"Aina ya makocha kama yule wa Yanga ambaye amefukuzwa ni miongoni mwa makocha ambao hawawezi kufanya kazi Ulaya kwani hakuwa na maneno mazuri kwa waandishi pamoja na vitendo vyake.

"Kwa kuwa amefukuzwa basi ni wazi kuwa akipata timu sehemu nyingine hawezi kudumu, ili uwe kocha mzuri ni lazima uwe na nidhamu katika kile unachoongea," amesema. 


4 COMMENTS:


  1. Mpaka sasa Zahera ndie kocha bora kuliko wote waliowahi kuwa nao Yanga. Yeye hakuwa kocha tu lakini yeye alikuwa mlezi wa timu na wachezaji hasa pale Yanga ilipoingia Katika shida ya mapato na sote tulishuhudia aliyoyafanya. Angekuwa wakati ule na wachezaji wa tuwi la kwannza angefanya makubwa sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. ko mlitaka na eymael awe anawalea kama zahera hahahahahaha

      Delete
  2. Duuuuuhhh!!!! Ange......... kumbe wakati mwingine hutumika vizuri. Zahera ange.......

    ReplyDelete
  3. Huyu hana tofauti na Steve Nyerere

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic