ABBAS
Tarimba, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, amesema kuwa mafanikio
makubwa ya kampuni hiyo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano
wanaoupata kutoka kwa wadau wake wa karibu ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Global
Publishers.
Tarimba
ameyasema hayo leo, Julai 27 alipotembelea Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza,
Mori Dar es Salaam ambapo ziara hiyo imekuja katika kutimiza miaka mitatu kwa
Kampuni ya SportPesa Tanzania.
“Tumekuwa
tukifanya kazi kwa ukaribu na watu mbalimbali na tulianza taratibu kwani kulikuwa kuna kampuni nyingine ambazo zinafanya kazi ila kwa ushirikiano mkubwa
ambao tumekuwa tukiupata kutoka kwa wadau pamoja na Kampuni ya Global hasa kwa
upande wa magazeti ya michezo ambayo ni Championi na Spoti Xtra tumefanikiwa
kwa kiasi kikubwa.
“Mbali na
kufanya kazi kwa mafanikio makubwa pia tumekuwa tukilipa kodi kwa Serikali
zaidi ya bilioni, hivyo sio kitu kidogo hasa ukizingatia kwamba maendeleo ya
Serikali yanahitaji kodi nasi pia tumekuwa tukilipa kodi.
“Wadau ambao
wapo pamoja nasi tunawaomba ushirikiano wao kwani bado tunazidi kupambana ili
kuwa bora na mambo yote tunayafanya kwa weledi na kuzingatia kanuni ambazo
zipo,” amesema Tarimba.
Mbali na
kusema hayo, Tarimba aliongeza kuwa amekuwa akiyafuatilia magazeti ya michezo
yanayochapishwa na Global Group ambayo ni Championi na Spoti Xtra, huku
akiwasihi waandishi wazidishe juhudi zaidi.
“Nimekuwa
nikiyafuatilia magazeti ya michezo ya Championi na Spoti Xtra, mbali na kwamba
ni washirika wetu ambao tunafanya nao kazi kwa ukaribu bado magazeti haya
yamekuwa na muonekano bora, ubora wa kazi pamoja na yale yanayoandikwa hivyo
cha msingi ni kushikilia hapo ili kuzidi kuwa bora zaidi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment