July 25, 2020

BAADA ya kupoteza kwa mara ya Kwanza akiwa ameongoza timu ya Namungo FC kwenye mechi 20 alizoziongoza mfululizo hivi karibuni, Kocha Mkuu Hitimana Thiery amesema kuwa bado wanashangaa kwa nini walifungwa mabao hayo.

Mara ya mwisho Namungo kupoteza ilikuwa ni Uwanja wa Taifa ilipofungwa mabao 3-2. Kwenye mchezo wake wa juzi, Namungo FC ilichapwa mabao 3-0 mbele ya Mbao FC, Julai 22, Uwanja wa Kirumba.

Akizungumza na Saleh Jembe,  Thiery amesema kuwa:"Sijui ilikuaje kwa kweli maana mimi nilishangaa hata wachezaji wenyewe walikuwa hawaelewi nini kimetokea ndani ya mchezo ule mbele ya Mbao.

"Baada ya mchezo kuisha tulikuwa na kikao na wachezaji pamoja na viongozi ili kuona namna gani walikuwa kwenye mchezo wetu uliopita hivyo tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Alliance, " amesema Thiery.

Julai 26, Alliance iliyo nafasi ya 18 itamenyana na Namungo iliyo nafasi ya nne ikiwa na pointi 64 zote zikiwa zimecheza mechi 37.

Alliance haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi huku Namungo wakiwa na uhakika wa kubaki ndani ya ligi.

1 COMMENTS:

  1. Don't be surprised of defeat my friend Hitimana. We must understandthat there is no joy in victory if you don't test the bitterness of defeat.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic