July 25, 2020

KUTOKANA na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kusema anabebeshwa mzigo wa lawama kwa mambo yasiyomhusu kwa kudaiwa kuwa anaihujumu timu, Saleh Jembe amesema kuwa kuna umuhimu wa Yanga kumaliza tofauti zao.

"Tunajua kwamba Frederick Mwakalebela anajua masuala ya mpira na ana uzoefu kitaifa na kimataifa kwa sasa anapaswa apunguze jazba pamoja na hasira ili afanye kazi yake kwa umakini.

"Yanga inabidi iunganishe nguvu kuelekea kwenye masuala ya usajili, kwa sasa tunajua kwamba nini ambacho watakipata ikiwa watauvunja uongozi wakati huu? 

"Kipi ambacho wanakihitaji mpaka Mwakalebela aihujumu timu kwa ajili ya Lipuli? Tunatambua kwamba Mwakalebela ni mtu wa Iringa amewahi kugombea ubunge na amekuwa ni mtu muwazi sasa akiihujumu mbele ya Lipuli Yanga inasaka nini kama ni ubingwa imeshapoteza na mataji mengine yamepita sioni kama Mwakalebela anaweza kuihujumu Yanga kwa lipi?" Saleh Jembe kuhusu ishu ya Fredrik Mwakalebela.

3 COMMENTS:

  1. Tatizo mpaka sasa kipigo cha mnyama kimeivuruga yanga mpaka viongozi na wachezaji hawana maelewano

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tuliwaambia hicho kigoli kimoja kitajibiwa kwa kishindo mpaka watatafutana

      Delete
  2. Wanamtafuta mchawi lskini hayupo. Mchawi labda ni kiwsngi kibovu cha timu yao.Afadhali wakubali ukweli kuliko visingizio visivyo na kichwa wala migumu. Sasa wamekuja na neno jipya makandokando!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic