July 25, 2020



MSHAMBULIAJI wa Lipuli Daruesh Saliboko, amesema kuwa ataendelea kumuenzi hayati, Benjamin Mkapa, rais wa awamu ya tatu ambaye alifariki jana, Julai 24.

Kesho Julai 26 kwa mujibu wa Serikali kutakuwa na taratibu za kuuaga mwili wa Mkapa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko mwenye mabao 11 kibindoni amesema kuwa enzi za uongozi wa Mkapa yeye alikuwa bado mdogo lakini ameshuhudia mengi yakitendeka.

 "Zama za uongozi wake nilikuwa mdogo sana lakini nilikuwa ninaona juhudi zake hasa kwa kuwa karibu na jamii, pia nimekuwa mkubwa nimeuona Uwanja wa Taifa na nimeutumia pia ni juhudi zake,ni pengo kubwa lakini sisi sote ni wa Mungu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic