July 19, 2020



UONGOZI wa Simba umesema kuwa wachezaji wake wote ndani ya kikosi chao wanauwezo wa kucheza kikosi cha kwanza kwenye timu yoyote Bongo ikiwa ni ndani ya Yanga pamoja na Azam FC kutokana na ubora walionao.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa sababu hiyo inawafanya nyota wao ikiwa ni pamoja na Ibrahim Ajibu na Sharaf Shiboub kusugua benchi licha ya uwezo mkubwa walionao.

“Ukimchukua Ajibu na Shiboub hawa hawana uwezo wa kukaa benchi kwenye timu zote hapa ukianzia Azam FC, nenda Yanga lazima waanze, ila kwa Simba wanapata tabu kwa kuwa kila mchezaji anajua, fikiria mchezaji kama Deo Kanda anakaa benchi, Kagere naye kuna mechi anakaa benchi hicho ndicho tunachotaka tunatoa chuma tunaingiza chuma.

"Hakuna asiyejua uwezo wa Ajibu nami pia ninamkubali kwani alipokuwa Yanga alikuwa ni staa wao na alikuwa ana uhakika wa namba ila kwa sasa ndani ya Simba kila mchezaji ni staa na ana uwezo mkubwa” amesema.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 35, Ajibu amecheza jumla ya mechi 19 na amefuga bao moja huku Kanda akicheza mechi 18 na kufunga mabao 7 na Shiboub amecheza 20 huku akitupia mabao mawili.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic