UWANJA wa Samora, uliopo Iringa leo, Julai 19 Lipuli FC iliyo chini ya Nzeyimana Mailo itaikaribisha Azam FC
inayonolewa na Aristica Cioaba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaokuwa ni
vita ya kupambania nafasi.
Mailo anazisaka pointi
tatu ili kujinusuru kwenye hatari ya kushuka daraja kwani kikosi chake kipo
nafasi ya 18 ikiwa na pointi 40 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 65
na ina hitaji kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili.
Mailo amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Azam FC na watapambana
kupata pointi tatu muhimu.
"Wachezaji wapo na morali kubwa ya kusaka matokeo na tumejipanga kuona kwamba tunafikia malengo yetu ya kubaki ndani ya ligi hivyo ni muhimu kwetu kushinda," amesema.
Zakaria Thabit, Ofisa
Habari wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo
wao dhidi ya Lipuli.
"Ni mchezo mgumu na wenye ushindani na kila timu inahitaji matokeo hivyo kwa maandalizi yetu kila kitu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wetu muhimu," amesema.
Mchezo wa kwanza
walipokutana Uwanja wa Taifa, Azam ilishinda kwa mabao 2-0.
Kinara wa kucheka na nyavu kwa Azam FC ni Obrey Chirwa mwenye mabao 12 huku Lipuli akiwa ni Paul Nonga mweye mabao 11.







0 COMMENTS:
Post a Comment