July 26, 2020


KLABU ya Simba imedhamiria kusajili kikosi cha kimataifa baada ya kuwa katika mchakato wa kusajili beki kutoka Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo imejihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao ambapo uongozi wa timu hiyo tayari umeshaweka wazi kutaka kufanya usajili kabambe wa wachezaji wa kimataifa ili kuleta ushindani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, Patrick Gakumba amesema kuwa, kuna mazungumzo kati yake na uongozi wa Simba juu ya kushusha beki kutoka TP Mazembe ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

“Nipo katika mazungumzo na viongozi wa Simba juu ya kuwaletea beki mwenye kiwango cha juu ambapo tayari nimeshampata beki huyo anayekipiga katika Klabu ya TP Mazembe japokuwa siwezi kumtaja kwa sasa ni nani kwa kuwa sheria inanikataza kumtaja mchezaji akiwa bado hajasaini.

“Mipango ikikamilika Simba watamsajili beki kutoka TP Mazembe ambaye ana uzoefu mzuri katika mashindano ya kimataifa kwani timu yake hiyo imeshawahi kufika fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mazungumzo yanakwenda vizuri kati yangu na uongozi wa Simba na mambo yakikaa sawa basi nitamuweka wazi mchezaji huyo na dau watakalotumia kumsajili,” alisema Gakumba.

Chanzo:Championi

3 COMMENTS:

  1. mpk wazeeke ndomunawafwata munajua kua mazembe awawez kuwaitaj tena ndomana munawafwata

    ReplyDelete
    Replies
    1. hao hao wazee si ndio wamekupiga 4G sasa unalalamika nini? kuwa mpole alafu angalia ujio wa mnyama 2020/2021 mtachapana sana bakora hapo Jangwani kama unawaona hao Tp mazembe wa ajabu mbona walimtaka Ajibu, mbona wamewasajili wakina Singano, Ambukile tatizo mtu akiwkwambia akili zako kama za mashabiki wa utoporo pigana akili zenu zinafanana kama madereva wa bodaboda

      Delete
  2. kuna ubabaishaji mkubwa sana kule kwao imefika hatua wachezaji wao wanagoma kuongeza mikataba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic