July 26, 2020



UWANJA wa Samora, majira ya saa 10:00 jioni leo kunatarajiwa kuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Lipuli na Yanga huku rekodi zikiwabeba wana Jangwani.

Lipuli iliyo chini ya Nzeyimana Mailo tangu ilipopanda daraja msimu wa 2017/18 imekutana mara tano kwenye mechi za ligi,Yanga imeshinda mechi tatu na Lipuli imeambulia ushindi mara moja na kuambilia sare moja.

Yanga imefunga jumla ya mabao sita huku Lipuli ikifunga jumla ya mabao matatu na kufanya jumla mabao kuwa tisa.

Matokeo yao yalikuwa namna hii: 2017/18, Lipuli 0-2 Yanga, Yanga 1-1 Lipuli msimu wa 2019/20, Lipuli 1-0 Yanga, Yanga 1-0 Lipuli na msimu wa 2019/20, Yanga 2-1 Lipuli.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo Lipuli inahaha kusaka tiketi ya kubaki ndani ya ligi huku Yanga ikipambania nafasi ya pili.

Lipuli ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 44 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 69 sawa na Azam FC ambayo ipo nafasi ya pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic