July 26, 2020


MICHAEL Sarpong, inaelezwa kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Rayon Sports ya Rwanda, Mghana, Michael Sarpong, amekubali kujiunga na miamba ya soka nchini Bongo, Simba.

Nyota huyo inaelezwa amekubali kujiunga na Klabu ya Simba kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya uongozi wa timu hiyo kukamilisha mazungumzo na wakala wake, huku dau lake likitajwa kuwa ni Sh milioni 138.


Sarpong alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ila mwisho wa siku wamepotezwa kutokana na dau la nyota huyo kuwa kubwa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa masuala ya usajili kwa Yanga kwa sasa mambo bado kwa kuwa wana mchezo mkononi hivyo hawana presha.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Masingisa amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia masuala ya tetesi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic