July 12, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna namna yoyote itakayowazuia kuifunga Yanga Uwanja wa Taifa licha ya kuwa wapinzani wao wapo vizuri na wana wachezaji wenye majina makubwa ambao wanaweza kuamua ushindi.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wana uwezo ndani ya Yanga ni pamoja na kiungo wao mshambuliaji Bernard Morrison ila mvurugano wa hivi karibuni unamshangaza.

Leo Simba inakutana na Yanga, kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ambapo mshindi atapata nafasi ya kukutana na Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery ambayo ilishinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars, Uwanja wa Mkwakwani.

"Kuna mambo magumu ambayo yanaweza kutokea duniani kwa sasa ikiwa ni pamoja na Simba hii iliyotwaa ubingwa kufungwa na Yanga, nakubali kwamba tunaweza kufungwa kwa maajabu ya Mungu hasa ukizingatia kwamba mpira ni dakika 90 lakini kwa ubora wa kikosi hapana.

"Ukitazama wapinzani wetu naona wana wachezaji wazuri lakini bado naona bado hasa ukizingatia kwamba hivi karibuni nimeskia kwamba mchezaji wao alishika kisu sijui kafanyaje nadhani kuna tatizo katika hili.

"Pia hata kama uliangalia mchezo wao wa ligi uliopita alipofunga bao hakushangilia hivyo kuna tatizo lipo lakini tuachane na hayo nasema sisi ni mabingwa hatuna cha kupoteza ila tunahitaji ushindi.

"Mashabiki waje ila wasisahau kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali katika kufuata kanuni za afya dhidi ya Corona, kisha kazi itaonyeshwa kwa wachezaji ndani ya uwanja namna mambo yatakavyokuwa.

"Kwenye maisha yangu ya soka hivi karibuni sijawahi kwenda kambi ya Simba lakini kutokana na umuhimu wa mechi hii dhidi ya Yanga nilipata nafasi ya kwenda kuwatembelea wachezaji na nilizungumza nao hivyo ninaamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa.

"Tulichowaambia wachezaji ikiwa ni kwamba hatuhitaji kitu chochote sisi, mashabiki hawana wanachohitaji chochote kinachohusiana na sababu zaidi ya kupata ushindi sisi ni mabingwa lazima tucheza kibingwa.

"Kwa Simba yenye Clataus Chama, Meddie Kagere, Luis halafu unapoteza itakuwa ajabu kwetu ujue" amesema. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic