July 25, 2020

MOHAMED Hussein 'Tshabalala', nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo, unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2,2020.

Fainali hiyo yenye ushindani mkubwa inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Akizungumza na Saleh Jembe,  Tshabalala amesema kuwa wameshakamilisha suala la kutwaa ubingwa jambo ambalo limebaki ni kutwaa taji la Shirikisho. 

"Tumekamilisha suala la kutwaa ubingwa hivyo tuna jukumu la kucheza mchezo wetu wa fainali dhidi ya Namungo ambao ni fainali ya Kombe la Shirikisho.

"Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na nina amini tutakamilisha malengo yetu, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema. 

Simba ilitinga hatua ya fainali baada ya kushinda mabao 4-1 mbele ya Yanga huku Namungo FC ikktinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic