July 25, 2020


LUC Eymael,  Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa amekuwa akibebeshwa lawama nyingi kuhusu mchezaji wake Bernard Morrison ambaye amebadilika ghafla na kuwa na tabia za utovu wa nidhamu. 

Morrison kwa sasa hayupo na kikosi cha Yanga ambacho kimewasili Iringa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli unaotarajiwa kuchezwa Julai 26, Uwanja wa Samora.

Tangu Julai 12 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho,  hatua ya nusu fainali Morrison alipotolewa dakika ya 64 alisepa na bodaboda na hajarejea ndani ya Yanga.

Mvutano mkubwa kati yake na Yanga ni kuhusu kandarasi yake ambapo yeye anasema dili lake limeisha huku Yanga wakieleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili.

Eymael amesema kuwa amekuwa akilaumiwa na watu wa Yanga kwa kuwa yeye alihusika kumleta nyota huyo ndani ya Yanga.

"Kweli nilimpendekeza aje kwa kuwa ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa na nilimkubali ila sikujua kama angebadilika namna hii kwangu ni mbaya.

"Napewa mzigo mzito wa lawama ni jambo gumu kwangu kwa kweli sihusiki,"

1 COMMENTS:

  1. Usihuzunike kwani Hao jamaa ndio walivo. Wewe ulimpenda na wao pia walimponda kuliko wewe lakini yale mapenzi yaliyokuwa yakijirudia usiku na mchana kwa lile goli alilowafunga watani yakafikia mwisho pale timu yangu ilipochapwa goli nne na ikawa unabebeshwa kila kitu. Vumilia ikiwa utaiweza. Kama hayo ndiyo yaliyomkuta Zahera ambae alikuwa kipenzi kikubwa na kuifanya timu makubwa kwa hali na mali ambayo hapana kocha yeyote aliewahi kuifanyia na akaja kungolwa ka jino bovu. Huko aliko anajichekea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic