July 25, 2020

UNAI Emery, Kocha Mkuu wa zamani wa Klabu ya Arsenal aliyemuachia mikoba yake Mikel Arteta ambaye bado anapambana ndani ya kikosi hicho amepata dili la miaka mitatu ndani ya Klabu ya Villarreal.

Raia huyo wa Hispania hakuwa na kazi tangu mwezi Novemba alipoachana na washika bunduki hao ndani ya Ligi Kuu England. 

Sasa anaanza maisha ndani ya La Liga ambapo anabeba mikoba ya Javier Camkeja ambaye alikiongoza kikosi hicho kumaliza nafasi ya tano.

Emery alitua ndani ya Arsenal akichukua mikoba ya Arsene Wenger Mei 28,2018 aliweza kufika na timu hiyo fainali ya Europa na alimaliza Ligi Kuu England akiwa nafasi ya tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic