August 10, 2020

 


KIKAO cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti, Elias Mwanjala, kimemalizika jioni hii ya leo.

Agosti 10 kulikuwa na kesi ya kuskilizwa kuhusiana na suala la kiungo mchezaji wa Yanga ambaye yupo kwenye mvutano na uongozi wa timu yake kwenye suala la mkataba.

Kuanzia asubuhi ya leo mpaka jioni kikao kilikuwa kikiendelea  lakini hakuna maamuzi yoyote rasmi yaliyotangazwa kwa Waandishi wa Habari waliokuwepo viunga vya TFF, Karume, Jijini Dar Es Salaam.

Wadau wengi wa masuala ya michezo walijitokeza makao makuu ya TFF hali iliyopelekea Polisi kuingilia kati kuweka ulinzi na usalama kwa raia.

Mvutano mkubwa upo kwenye mkataba ambapo mchezaji anasema kuwa alisaini kandarasi ya miezi sita huku Yanga wakieleza kuwa alisaini kandarasi ya miaka miwili.

Agosti 8, saa nane, Simba ilimtambulisha mchezaji huyo kuwa mali ya Simba jambo ambalo liliamsha hisia kwa Yanga ambao walitoa taarifa kwamba wanalifuatilia suala hilo kwa ukaribu.


16 COMMENTS:

  1. Tff iache siasa imeskilza pande zote 3 na vielelezo vyote vimewasilishwa na kila upande badala ya kufanya maamuz wanaendeleza siasa zile zile za simba ma yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama mchezaji mwenyewe hataki kuendelea kufanya kazi na Yanga kwanini Yanga wanatumia nguvu kubwa mwisho wa siku ni hasara tu.Maaana Morrison akifungiwa kucheza soka watakaothirika ni Yanga kwa kuwa watakuwa wamepoteza mchezaji wao.Ikiamuliwa kuchezea Yanga pia ni tatizo kwa Yanga kwakuwa mchezaji mwenyewe hataki kuichezea Yanga.ikiamuliwa Morrison achezee simba ni hasara kwa Yanga vile vile. La msingi naona Yanga wakae chini na Simba wafidiwe gharama zao kwa Morrisoni nadhani itakuwa winiwini situation. Mchezaji akiwa kwenye kandarasi ndani ya miezi sita 6 anahaki ya kufanya mazungumzo na klabu nyengine wanayanga mnatakiwa kufahamu hivyo.

      Delete
    2. Kama ataki si simba walipe pesa ya kumsajili kwa yanga kama ulaya tu ili aende kwao.Simba muna penda kitonga

      Delete
    3. Yani unawezaje kumfidia mtu asiyekuwa na mkataba, Morrison siyo chizi kusema yeye hajasaini mkataba wa miaka miwili na Yanga, na kama kweli alisaini mkataba huo kesi yake ilipelekwa mapema T.F.F kabla ya Simba kumtambulisha, T.F.F walishindwa nini kuamua kuwa ni mchezaji wa Yanga MUDA WOTE HUO

      Delete
  2. Hizo ni siasa za mpira wa Tz. Ukweli uwekwe wazi. Tatizo ni kuwa yako makando kando mengine kuhusu mkataba hata ule wa awali ni simba nao wamechochea moto.

    ReplyDelete
  3. Tatizo ni upenzi kwenye hii kamati. Elias Mwanjala aligombea uongozi Yanga ndio Mwenyekiti wa kamati. Hans Pope mjumbe wa kamati ni Simba. Kamati nzima imemeguka kwa upenzi.Amueni haki.

    ReplyDelete
  4. Hii issue inatishia amani baina ya wapenzi wa soka wa Tanzania

    ReplyDelete
  5. Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ukweli utajulikana tu,hii issue maamuzi yatakapotolewa hata Kama Kuna upande haujaridhika bado Kuna rufaa Hadi FIFA. Hivyo Ni jambo la subira tu hapa. binafsi ningependezwa Kama swala hili lingekuwa FIFA Cse huko hakuwezi kuwa na lawama kwamba TFF wamependelea upande fulani.

    ReplyDelete
  6. Issue hii inaweza kwenda FIFA.

    ReplyDelete
  7. Pande ni 2 tu Yanga na Morisson aliyeshtaki.Haki itendeke.

    ReplyDelete
  8. Hii TFF ya mwaka gani jamani?
    Yaani issue ya mkataba wa mchezaji mpaka ziletwe documents na kikao kifanyike siku mbili!
    Inamaana huo mkataba haukusajilwa TFF?
    Kwa uelewa wangu mdogo Hilo Jambo lilikua ni la jutamka tu, kwamba anamkata na Yanga au la. Kwa maana kila kitu kipo mezani na kwenye mtandao.

    ReplyDelete
  9. Nasi tunawashutumu TFF kwa ushabiki, tunataka maamuzi yatoke kwa ushabiki wetu sio kimamlaka

    ReplyDelete
  10. hahahaha tifuatifua h hata siielew hz sheria wanaztoa wap

    ReplyDelete
  11. Acheni mbwembwe yusubiri maamuzi ndo tuongee

    ReplyDelete
  12. You can use force to to drag the donkey to the river, but you can't use similar method to make him drink the water

    ReplyDelete
  13. Kinachonishanga haya matatizo yamekuwa yakijirudia lakini hawasemi yanaishia wapi
    Kabwili alidai alitaka kuhongwa lakini mpaka leo bado swala halijatolewa maamuzi.
    Kuna issue ya Mwakalebela kutaka kumsaini Chama akiwa ndani ya mkataba mpaka leo maamuzi hayajatoka
    Kuna issue ya mwamuzi aliyechezesha yanga na kagera mpaka leo maamuzi hayajatoka
    Kama rais wa tff angekuwa makini angeshavunja hizi kamati

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic