Agosti 10 kulikuwa na kesi ya kuskilizwa kuhusiana na suala la kiungo mchezaji wa Yanga ambaye yupo kwenye mvutano na uongozi wa timu yake kwenye suala la mkataba.
Kuanzia asubuhi ya leo mpaka jioni kikao kilikuwa kikiendelea lakini hakuna maamuzi yoyote rasmi yaliyotangazwa kwa Waandishi wa Habari waliokuwepo viunga vya TFF, Karume, Jijini Dar Es Salaam.
Wadau wengi wa masuala ya michezo walijitokeza makao makuu ya TFF hali iliyopelekea Polisi kuingilia kati kuweka ulinzi na usalama kwa raia.
Mvutano mkubwa upo kwenye mkataba ambapo mchezaji anasema kuwa alisaini kandarasi ya miezi sita huku Yanga wakieleza kuwa alisaini kandarasi ya miaka miwili.
Agosti 8, saa nane, Simba ilimtambulisha mchezaji huyo kuwa mali ya Simba jambo ambalo liliamsha hisia kwa Yanga ambao walitoa taarifa kwamba wanalifuatilia suala hilo kwa ukaribu.








Tff iache siasa imeskilza pande zote 3 na vielelezo vyote vimewasilishwa na kila upande badala ya kufanya maamuz wanaendeleza siasa zile zile za simba ma yanga
ReplyDeleteKama mchezaji mwenyewe hataki kuendelea kufanya kazi na Yanga kwanini Yanga wanatumia nguvu kubwa mwisho wa siku ni hasara tu.Maaana Morrison akifungiwa kucheza soka watakaothirika ni Yanga kwa kuwa watakuwa wamepoteza mchezaji wao.Ikiamuliwa kuchezea Yanga pia ni tatizo kwa Yanga kwakuwa mchezaji mwenyewe hataki kuichezea Yanga.ikiamuliwa Morrison achezee simba ni hasara kwa Yanga vile vile. La msingi naona Yanga wakae chini na Simba wafidiwe gharama zao kwa Morrisoni nadhani itakuwa winiwini situation. Mchezaji akiwa kwenye kandarasi ndani ya miezi sita 6 anahaki ya kufanya mazungumzo na klabu nyengine wanayanga mnatakiwa kufahamu hivyo.
DeleteKama ataki si simba walipe pesa ya kumsajili kwa yanga kama ulaya tu ili aende kwao.Simba muna penda kitonga
DeleteYani unawezaje kumfidia mtu asiyekuwa na mkataba, Morrison siyo chizi kusema yeye hajasaini mkataba wa miaka miwili na Yanga, na kama kweli alisaini mkataba huo kesi yake ilipelekwa mapema T.F.F kabla ya Simba kumtambulisha, T.F.F walishindwa nini kuamua kuwa ni mchezaji wa Yanga MUDA WOTE HUO
DeleteHizo ni siasa za mpira wa Tz. Ukweli uwekwe wazi. Tatizo ni kuwa yako makando kando mengine kuhusu mkataba hata ule wa awali ni simba nao wamechochea moto.
ReplyDeleteTatizo ni upenzi kwenye hii kamati. Elias Mwanjala aligombea uongozi Yanga ndio Mwenyekiti wa kamati. Hans Pope mjumbe wa kamati ni Simba. Kamati nzima imemeguka kwa upenzi.Amueni haki.
ReplyDeleteHii issue inatishia amani baina ya wapenzi wa soka wa Tanzania
ReplyDeleteHakuna marefu yasiyo na ncha. Ukweli utajulikana tu,hii issue maamuzi yatakapotolewa hata Kama Kuna upande haujaridhika bado Kuna rufaa Hadi FIFA. Hivyo Ni jambo la subira tu hapa. binafsi ningependezwa Kama swala hili lingekuwa FIFA Cse huko hakuwezi kuwa na lawama kwamba TFF wamependelea upande fulani.
ReplyDeleteIssue hii inaweza kwenda FIFA.
ReplyDeletePande ni 2 tu Yanga na Morisson aliyeshtaki.Haki itendeke.
ReplyDeleteHii TFF ya mwaka gani jamani?
ReplyDeleteYaani issue ya mkataba wa mchezaji mpaka ziletwe documents na kikao kifanyike siku mbili!
Inamaana huo mkataba haukusajilwa TFF?
Kwa uelewa wangu mdogo Hilo Jambo lilikua ni la jutamka tu, kwamba anamkata na Yanga au la. Kwa maana kila kitu kipo mezani na kwenye mtandao.
Nasi tunawashutumu TFF kwa ushabiki, tunataka maamuzi yatoke kwa ushabiki wetu sio kimamlaka
ReplyDeletehahahaha tifuatifua h hata siielew hz sheria wanaztoa wap
ReplyDeleteAcheni mbwembwe yusubiri maamuzi ndo tuongee
ReplyDeleteYou can use force to to drag the donkey to the river, but you can't use similar method to make him drink the water
ReplyDeleteKinachonishanga haya matatizo yamekuwa yakijirudia lakini hawasemi yanaishia wapi
ReplyDeleteKabwili alidai alitaka kuhongwa lakini mpaka leo bado swala halijatolewa maamuzi.
Kuna issue ya Mwakalebela kutaka kumsaini Chama akiwa ndani ya mkataba mpaka leo maamuzi hayajatoka
Kuna issue ya mwamuzi aliyechezesha yanga na kagera mpaka leo maamuzi hayajatoka
Kama rais wa tff angekuwa makini angeshavunja hizi kamati