August 26, 2020

 


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Larry Bwalya, ameikamua timu hiyo Sh milioni 138 kama ada ya usajili akisaini mkataba wa miaka miwili.

 

Bwalya amejiunga na Simba akitokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia akiwa mchezaji wa pili kutoka taifa hilo kuichezea Simba baada ya Clatous Chama.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Spoti Xtra limezipata ni kuwa, kiungo huyo amekubali kujiunga na Simba baada ya makubaliano ya kupatiwa dola 60,000 (sawa na Sh 138,565,000) kama sehemu ya usajili wake.

 

“Bwalya yeye amejiunga na Simba kwa dau la dola 60,000 kutokana na makubaliano yake, timu na wakala ambaye amesimamia dili hilo hadi amejiunga na Simba.

 

“Nadhani hiyo siyo pesa ndogo kwa sababu ukiangalia ni zaidi ya milioni mia, naamini atakuwa msaada ndani ya Simba hasa kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa, lakini akiwa ni mchezaji chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Zambia,” kilisema chanzo chetu.


1 COMMENTS:

  1. kwa kiwango cha bwalya hyo pesa ni ndogo jamaa anajua sna

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic