Mpaka sasa
kwa timu ambazo zimejipanga kufanya usajili ninaona kwamba zimeweza kufanya
kile ambacho zinahitaji jambo ambalo katika hilo sina mashaka nalo .
Jambo la
msingi ambalo linapaswa kuzingatiwa katika usajili ambao unafanywa ni kufuata
ripoti ya mwalimu, yeye ndiye ambaye anajua kwamba anahitaji aina gani ya
wachezaji kwenye kikosi chake.
Wapo wale
ambao watafanya usajili kwa kufuata mahitaji yao hilo lipo wazi kwa kuwa ni
mambo ambayo yapo kwenye soka letu la Bongo.
Zama hizo muda wake umekwisha halipaswi lipewe nafasi kwa sasa.
Muda wa
kufanya kazi kwa utaalamu na kufuata taaluma ya kazi ya mpira ni sasa. Soka
letu linazidi kukua kwa kasi ikiwa masuala ya kufanya maamuzi kwa kuwa wewe ni
kiongozi haileti picha nzuri kwa afya ya soka letu.
Timu zote
ambazo zitafanya usajili kwa mapendekezo yao binafsi wakati wa kujua masuala
hayo yanakuja, mchezo wa mpira hauhitaji
mambo mengi zaidi ya vitendo na data ambazo zinaongea ukweli muda wote.
Ndani ya
dakika 90 ni muda sahihi uwanjani ambao utatosha kuaminisha mashabiki na
wanachama wa timu kwamba huyo aliyeletwa ndani kucheza ni pendekezo la kocha
ama kiongozi.
Sababu moja
kubwa itakayofanya atambulike kwamba alisajiliwa kwa presha ama chaguo la
kiongozi ni muda wake atakaoutumia ndani ya uwanja na kile ambacho atakionyesha
pia pale atakapopata muda.
Ipo wazi
kwamba kuna wale wachezaji ambao walipata nafasi ya kusajiliwa kwa msimu wa
2019/20 ndani ya timu mbalimbali hawakuwa na nafasi kwenye timu zao mpaka msimu
unaisha.
Rekodi
zinaonyesha kwamba wapo wachezaji ambao walisajiliwa na timu zao kwa msimu wa
2019/20 na hawajacheza mchezo hata mmoja ndani ya ligi zaidi ya kuishia benchi.
Hii ni
mbaya na inatoa picha kwamba hakukuwa na chaguo la mchezaji huyo ndani ya
kikosi, pia inaua uwezo wa mchezaji na kurudisha nyuma maendeleo ya soka hasa
ikiwa alichukuliwa kutoka kwa timu ambayo ilikuwa inahitaji huduma yake labda
kutokana na uchumi kuyumba wakashindwa kubaki na mchezaji.
Kwa
viongozi wa timu pia ni somo kwamba mpira wa sasa unahitaji fedha na uwekezaji
mkubwa hivyo wanajukumu la kuongeza vyanzo vyao vya mapato ili kuweza kubaki na
wachezaji ambao wanawahitaji pale msimu unapokwisha.
Tukiachana
na timu na mchezaji pia ana kazi ya kuangalia nafasi yake kule anakokwenda
asifikirie kupata mkwanja huku nafasi yake ya kucheza akiiweka kapuni
itampoteza kwenye ramani ya mpira.
Kwa kuwa
maisha ya soka lazima yaendelee mchezaji mmoja kutoka na kwenda kwenye timu
nyingine ni muda sahihi wa kila mchezaji ambaye anakwenda kuanza maisha mapya.
Imani yangu
ni kwamba mpaka pale dirisha la usajili litakapofungwa Agosti 31 kila kitu
kitakuwa kimekwenda sawa ndani ya timu zote kuanzia zile za Ligi Daraja la
Kwanza, Daraja la Pili,Ligi ya Wanawake pamoja na zile zinazoshiriki Ligi Kuu
Bara.
Kila mtu atavuna
kile atakachokipanda ndani ya uwanja ni wakati wa kuanza maandalizi kwa timu
zote kwani muda wa ligi kuanza upo njiani na muda wa dirisha la usajili
kufungwa upo karibu.
Ujumbe
wangu kwa timu ambazo zimepanda daraja kwa msimu wa 2019/20 zikiwa na uhakika
wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 zinapaswa zijipange kwelikweli
kuleta ushindani.
Gwambina FC
na Dodoma Jiji hizi zilipanda jumlajumla kutoka Ligi Daraja la Kwanza huku
Ihefu wao wakiweka rekodi ya kushinda mchezo wa playoffs mbele ya Mbao FC wote
wanapaswa pongezi lakini wasijisahau.
Kama
ambavyo wamepishana na Singida United,Lipuli FC,Ndanda FC,Alliance na Mbao
wajifunze kwamba msimu ujao isije ikawa ni zamu yao kuwapisha wengine.
Yote kwa
yote wasisahau kwamba makosa makubwa ya timu kupata ushindi ni kwenye
maandalizi na usajili hivyo wanapaswa kuwa bora katika usajili wakati huu ambao
unaelekea ukingoni pamoja na kuanza maandalizi mapema kujenga timu zao.
Nimeona
Gwambina FC wao washamaliza kufanya usajili ambapo wana mchanganyiko wa wachezaji
ikiwa ni pamoja na wale ambao walikuwa ndani ya timu pamoja na wazoefu kutoka
kwenye ligi kuu hiyo ni sawa kwa kuwa lazima mabadiliko yawepo.
Lakini
licha ya kumaliza kufanya usajili mzuri ni muhimu kuwa na mpango kazi makini
utakaofanya timu iwe inapata matokeo uwanjani na kuleta ushindani kama
ilivyokuwa ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.
Tunataka
kuona kila timu inafanya maajabu na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote
ambazo watacheza iwe nyumbani ama ugenini muhimu kupambana kupata matokeo.
Muda wa
kufikiria kwamba bado mpo Ligi Daraja la Kwanza umekwisha kwa sasa ni mapambano
ndani ya Ligi Kuu Bara ni muhimu kuweka dira mapema kabla mambo hayajaanza
kubadilika.
Mashabiki
wenu mtambue kwamba wanajua yapo matokeo matatu, kufungwa, sare na kushinda.
Furaha yao kubwa ipo kwenye kushinda basi pambaneni kuwapa mashabiki kile
ambacho wanahitaji.
Tunahitaji kuona kwamba msimu wa 2020/21 mnakuja kuleta kitu kipya ambacho ni ushindani bila kujali kwamba mmetoka kumaliza maisha yenu ndani ya Ligi Daraja la Kwanza bado mna nafasi ya kufanya vizuri.
Maandalizi
makini yanahitajika kwa ajili ya msimu mpya, usajili pia usipuuzwe
0 COMMENTS:
Post a Comment