RAIS wa Barcelona, Josep Bartomeu, amethibitisha kuwa Ronald Koeman atapewa kibarua cha kuwafunza miamba hao wa Catalan.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona amesaini dili la miaka miwili alicheza jumla ya mechi 305 na kufunga mabao 106.
Kwa sasa Koeman ni kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi, lakini Agosti 18 alikwenda Barcelona kukamilisha dili hilo na anatarajiwa kutangazwa juma hili.
Klabu ya Barcelona jana ilitangaza kumfuta kazi kocha wake, Enrique Setién Solar, ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa kwa kudhalilishwa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kichapo cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich.
Kuhusu uvumi kwamba nyota wa klabu hiyo, Lionel Messi, ataondoka, Bartomeu amesema, “Messi anataka kumalizia soka lake Barca, na amelisema hilo mara nyingi. Bado ana mkataba hadi 2010.”
Pamoja na hatua hiyo mpya, pia amedokeza kwamba timu yake itajengwa upya kwa upande wa wachezaji.
Mkataba hadi 2010 umekuwa mkataba wa manyani fc
ReplyDelete