August 11, 2020

 KWA sasa kinachoendelea kwenye masuala ya michezo ni sakata la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison ambaye ishu yake ipo kwenye Kamati ya Hadhi ya Wachezaji.


Kinacholeta mvutano ni suala la mkataba ambapo Morrison anasema kuwa alisaini dili la miezi sita huku Yanga ikieleza kuwa imempa kandarasi ya miaka miwili.

Pia Agosti 8 alitambulishwa ndani ya Simba huku habari zikieleza kuwa amesaini dili la miaka miwili.

Jana, Agosti 10 ilianza kuskilizwa kesi hiyo makao makuu ya Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) na leo Agosti 11 inaendelea kuskilizwa huu hapa ujumbe wa Saleh Jembe:-Mpunguze presha leo mapema itajulikana, ushauri tuipe kamati muda majibu yapatikane lakini vizuri usiingizwe kwenye zile PROPAGANDA...


"Majibu yakitoka sote tunajua kabaki Yanga au kapitishwa Simba, maisha yanaendelea...

"Kawaida watu wa Kamati wanazima simu kabisa hadi wanapomaliza kikao.

"Zile sijui Hans Poppe kaondolewa, sijui Yanga wamebanwa ACHANA NAZO," 


8 COMMENTS:

  1. Nilikuwa nakufuatilia sana Bin Zubeiry, lakini sitaki kukufuatilia tena kutokea leo

    ReplyDelete
  2. Naona umechanganya madawa.Huyu mwenye blog ni Saleh Ally Jembe sio Mohamud Bin Zubeiry.

    ReplyDelete
  3. mkataba una utata..
    ni rahisi kufikiria...Sydney, Balinya, Niyonzima, Ykipe, Molonga, Sibomana hawakupata miaka miwili...ndiyo ije Morrison apate kwa uwezo gani? kutembea juu ya mpira au kwa kumfunga simba.. Hadi kipindi mkataba utata unatayarishwa Morrison alikuwa na magoli mawili na assist mbili!

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa kama morisson hana uwezo wa mpira vipi simba wanamsajili kinguvu na kutaka kuhalalisha kisicho halali kwa kutumia kamati ambayo imejaa watu wa simba???
      ni kama suala la kutaka kuoa mke ambae ana mme na hajapewa talaka !!!!
      mtu alie muadilifu (shekhe abd padri) hawezi fungisha ndoa akijua hayo

      Delete
  4. kwa kweli Bongo soka lake lina tatazo kama mkataba wake ulikuwa na utata kwa nini alipata leseni ya kuitumikia Yanga hiki ni kichekesho kikubwa hawa tff wana akili kweli juzi hapa baada ya Morison kusema kacheza mechi mbili za mwanzo bila ya kuwa na mkataba tff waliruka kimanga kupinga hilo sasa iweje leo mnachezea watu akili zao kwa ufupi hamna jipya blablaaa nyingi tu inaonekana hamjui mfanyalo.

    ReplyDelete
  5. Mwenyekiti wa kamati lawyer Elias Mwanjala ndio sababu ya vurugu zote.Anajaribu kukalia ukweli ili kupendelea timu yake pendwa aliyegombea uongozi na kupigwa chini Amepigwa chini kwenye uchaguzi wa chama cha mpira mkoani Mbeya juxi Jumapili kwa kupata kura 4.Hana weledi wa kuongoza kamati nyeti kama hiyo ya haki ya TFF .

    ReplyDelete
  6. Kama Morrison anajinasibu hana mkataba kwanini alimpigia kocha luc akiomba kucheza mechi ya tarehe 12 July? Hivi mchezaji anayeituhumu klabu kufoji anawezaje kuiomba klabu yake hiyo anayoituhumu arejee kucheza??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic