LIVERPOOL imetangaza kuwa imemalizana na beki Kostas Tsimikas kutoka Klabu ya Olympiacos kwa dili la muda mrefu kwa dau linalotajwa kuwa ni pauni milioni 11.75.
Nyota huyo mwenye miaka 24 raia wa Ugiriki amekuwa kwenye ubora mkubwa licha ya kutokuwa na jina kubwa kwenye ulimwengu wa masuala ya michezo.
Kwenye Klabu ya Olympiacos tangu Desemba 2015 amecheza jumla ya mechi 86 ndani ya kikosi chake na amekabidhiwa jezi namba 21 atakayotumia msimu wa 2020/21.
Beki huyo amesema kuwa anafuraha kubwa kuingia kwenye maisha mapya ndani ya Ligi Kuu England ana imani kuwa atafanya makubwa licha ya jina lake kutokuwa kubwa.
"Ninafuraha kubwa kwa sasa kuanza maisha mapya ndani ya Liverpool ni ligi ngumu yenye ushindani ambayo inatazamwa na watu wengi duniani nami nitapambana ili kutimiza majukumu yangu.
"Kuna kazi nyingi za kufanya na kusimamia pia kwani kwangu ni fahari kuwa ndani ya timu bora ninapenda vingi ilikuwa ni ndoto yangu muda mrefu kuwa hapa na imetimia," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment