MTUPIAJI namba moja wa Simba, Meddie Kagere leo Agosti 21 amewasili nchini akitokea Rwanda alikokuwa kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Kagere ni mshambuiaji bora kwa msimu wa 2019/20 akiwa ametupia mabao 22 amekuwa na mwendelezo bora wa kutupia kwa kuwa msimu wa 2018/19 alitupia mabao 23.
Kwa muda wa misimu miwili, Kagere ametupia mabao 45 na kumfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji wenye urafiki na nyavu.
Kesho atakuwepo kwenye kilele cha tamasha la Simba day ambapo timu yake itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Vital,O ya Burundi.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kesho itakuwa ni siku ya burudani hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.
0 COMMENTS:
Post a Comment