RASMI mshambuliaji Michael Sarpong raia wa Ghana leo Agosti 21 ametua Bongo kwa ajili ya kumalizana na mabosi hao ambao wanaimarisha kikosi chao.
Sarpong yeye alikuwa anakipiga ndani ya Rayon Sports ya Rwanda na ametua leo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Habari zinaeleza kuwa dili lake la awali ambalo alisaini ilikuwa ni la miaka miwili.
Baada ya kutua Bongo Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Sarpong amesema kuwa amefurahi kwa mapokezi makubwa ambayo amepewa na anaamini atatimiza majukumu yake.
"Ninafurahi kwa mapokezi ambayo nimeyapata kutoka kwa mashabiki wangu, nami pia ninaahidi kuweza kupambana kwa ajili ya timu yangu kwenye mashindano yote.
"Ninaamini kwamba Yanga ni timu kubwa hilo lipo wazi hivyo ni muhimu kwangu pia kupambana kuweza kuyafikia malengo," amesema.
Hilo galasa Kama umempokea tupia picha. Mnaspeculate Sana hayupo kwenye list yetu
ReplyDeleteKwani hiyo hapo juu na nani kama sio yeye?
ReplyDeleteHalafu kupokea wachezaji wanakuwa wengi ila kwenye mechi zao huwaoni
ReplyDelete